Kamanda wa Jeshi la Polisi Tanga Edward Bukombe amewatahadharisha baadhi ya watu wanaotaka kufanya uhalifu kipindi cha Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kuacha kabisa kwani Jeshi hilo lipo kila kona kuhakikisha Watanzania wanafurahia Sikukuu kwa amani.
Kamanda ameyasema hayo ikiwa Waumini wa dini ya Kikristo wanasherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu.
Aidha Kamanda Bukombe amesema marufuku kwa Madereva wa magari ya abiria hata binafsi kuendesha magari wakiwa wametumia vilevi kwani watakapo tiwa nguvuni watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Changamoto utakazokutana nazo kushoot Music Video USA, Mtanzania kafunguka