Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ameagiza Madiwani kumi na moja waliokamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uvuvi haramu katika maeneo mbalimbali nchini kuripoti mara moja katika ofisi za Wizara hiyo ifikapo December 5 mwaka huu.
Mpina amewataka kuripoti Mjini Dodoma kabla Serikali haijachukua hatua zaidi ikiwa ni pamoja na kuziondolea Halmashauri hizo haki za kukusanya na kusimamia Rasilimali za Uvuvi.