Waziri wa Madini Angela Kairuki amesema ili kufikia malengo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo ambao unaelekeza kuwa ifikapo mwaka 2025 Tanzania iwe imefikia uchumi wa kati, sekta ya madini inalazimika kuongeza mchango katika pato la Taifa kutoka asilimia 4.8 ya sasa kufikia asilimia 10 mwaka 2025.
Waziri Kairuki amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Kongamono la Uwekezaji katika Sekta ya Madini kati ya Tanzania na China lililofanyika jijini Beijing nchini China.
Akifungua Kongamano hilo la kwanza la aina yake kuandaliwa na Wizara ya Madini kwa ushirikiano na Kituo cha Uwekezaji Tanzania na Ubalozi wa Tanzania nchini China, Waziri wa Madini Angela Kairuki, ametumia jukwa hilo kuelezea mipango ya wizara yake katika kukuza sekta ya madini nchini.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Geofrey Mwambe amesema, nia ya serikali katika maboresho ya Sera na Sheria ni kuhakikisha kuwa rasilimali za Tanzania zinawanufaisha Watanzania pamoja wawekezaji.
“Sheria zetu tulizozitengeneza ni za kutuhakikishia Sisi kama nchi pia tunapata, hela hizo tunataka ziende kwenye maji, barabara, hospitali na katika huduma zote” -Mwambe
Akikaribisha washiriki wa kongamano hilo balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki amesema serikali ya awamu ya tano imejipanga kutumia fursa za uwekezaji wakati wa Mkutano wa FOCAC uliofanyika Beijing mwezi September mwaka huu
Kwa upande wao Wawekezaji kutoka China ambao wamewekeza Tanzania na wawekezaji watanzania wameeleza kufurahishwa na mabadiliko yanayofanywa na Serikali katika Sekta ya madini lakini zaidi kuhusu kongamano hilo ambalo wamesema ni la faida.
WAZIRI KAIRUKI KWENDA CHINA ‘KUUZA’ MIRADI MADINI | “KILA ARDHI TZ INA MADINI”
WAZIRI LUGOLA AGEUKIA MAKANISA NA MISIKITI “MTAPATA CHA MTEMA KUNI”