Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amekutana na wadau wa mazingira na kujadili namna ya kutatua na kukabiliana na changamoto za viumbe vamizi.
Mkutano umeshirikisha wadau mbalimbali zikiwemo kamati za kudumu za bunge za kuduma za viwanda na biashara, maliasili, mazingira na mifugo na uvuvi.
Pia umeshirikisha wadau,wataalamu, watafiti kutoka vyuo mbalimbali, asasi za kiraia na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech).
“Tumefika mahali lazima tutafakari hatua za kinidhamu tutakazozichukua dhidi ya suala hili. Lengo la mkutano ni kulipigia kelele na kuonyesha ukubwa wa tatizo.”
” Naomba wataalamu na watafiti mfunguke kutoka moyoni nini kifanyike ili kukabiliana na viumbe hawa vamizi. Hii ni hatua ya kwanza na mawazo na mapendekezo yenu yatachukuliwa na kupeleka ngazi ya juu,” amesema Makamba
LIVE MAGAZETI: JPM ashtukia msamaha wa Kodi, Pigo la mwisho kwa Makonda