Leo September 11, 2018 Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema wananchi wasikubali kurubuniwa na baadhi ya watu wanaowadanganya kuchangia fedha ili kupata Milioni 50, zilizoahidiwa mwaka 2015 kipindi cha uchaguzi kwa kila kijiji na kwamba serikali haina fedha hiyo kwa sasa.
Makamu wa Rais Samia amezungumza hayo wakati akizungumza na wananchi katika kijiji cha Munzeze Halmashauri ya Buhigwe mkoani Kigoma nakuweka wazi kuwa, fedha zilizopo kwa sasa zinatumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo , ikiwemo elimu, afya, barabara, pamoja na maji lengo ikiwa ni kukuza maendeleo nchini.
Agizo la JPM lamfanya Mkurugenzi Arusha kuingia sokoni kukusanya kodi