Seikali imedhamiria kuhakikisha kuwa biashara za mipakani zinaimarishwa na kufanyika kwa ufanisi zaidi kwa kuondoa vikwazo vyote vya kikodi na visivyokuwa vya kikodi na kuwezesha Wananchi na Taifa kwa ujumla kunufaika na kukuza biashara.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Injinia Stella Manyanya wakati akitangaza utaratibu maalumu wa kuhudumia Wafanyabiashara za mipakani
“Katika kufikia malengo hayo, Wizara ya Viwanda na Biashara inapenda kuutaarifu Umma na Wafanyabiashara wote nchini hususan wale wanaofanya biashara mipakani kuwa, imeweka utaratibu maalum utakaowezesha kutoa taarifa juu ya vikwazo, changamoto au kero za kibiashara hasa zile zisizokuwa za kikodi (NTBs) wanazokumbana nazo” Naibu waziri
DOGO KAGERE VIPI SHULE, AMESHUKA AU? WALIMU “ANAJICHANGANYA NA WATU WAZIMA”