Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla amjibu mtoto wa Edward Lowassa, Fredick Lowassa kuhusu ujumbe aliopost leo January 29, 2018 katika kurasa zake katika mitandao ya kijamii.
“Mdogo wangu Fredrick Lowassa, tulia usiwe na hofu. Sikukurupuka kuhusu issue ya Mzee wako, Ndg. Edward Lowassa, kama ana kiwanja ama la, kwenye eneo la Plot No. 4091 Njiro Arusha. Ukweli ni kwamba nilichokisema ni kuwa ‘tusubiri tupate majibu toka kwa mamlaka inayohusika na kutoa hati za umiliki wa ardhi”-Kigwangalla
Kuna majina mengi makubwa yanasemwa, yakiwemo ya Mawaziri Wakuu wastaafu, Ndg. Frederick Sumaye na Ndg. Edward Lowassa, watumishi wa zamani wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na Bodi ya Utalii Tanzania, kuna Mkuu wa Mkoa wa zamani Ndg. Ole Njoolay anatajwa,”-Kigwangalla
“Kuna Waziri wa Zamani Ndg. Batilda Buriani, Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Ndg. Mshana Joseph na wengine wengi, lakini hatuwezi kuwahukumu ama kuwataja waziwazi kwa sasa mpaka tupate nyaraka maana inawezekana wanasingiziwa ama vipi’.-Kigwangalla
“Nimesikitishwa na matamshi kutoka kwa Waziri” – Lowassa