Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Issack Kamwelwe amesema uopoaji wa miili ya waliofariki Dunia baada ya kupinduka na kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere utakamilika leo Septemba 21, 2018.
Kamwelwe ameeleza hayo leo mchana wakati akihojiwa na kituo cha Utangazaji cha Taifa. Akiwa eneo la tukio Kisiwa cha Ukara wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.
Hadi kufikia sasa miili zaidi ya 125, imepatikana katika ajali hiyo kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.