Leo September 17, 2018 Chama cha Mapinduzi (CCM) kimezidi kung’ara jijini Mbeya baada ya kuzoa Kata zote tatu zilizokuwa zinafanya uchaguzi wa marudio kufuatia waliokuwa madiwani kupitia CHADEMA kutimkia chama hicho tawala.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika, Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Mbeya Mjini James Kasusura aliwatangaza wagombea wa CCM kuwa washindi.
Katika Kata ya Maanga alimtangaza, Newton Mwatujobe (CCM) kuwa mshindi kwa kupata kura 1897 na kumshinda, Steven Mwashilindi (CHADEMA) ambaye alipata kura 1703
Pia katika Kata ya Iwambi alimtangaza, Humphrey Ngalawa (CCM) kuwa mshindi kwa kuzoa kura 2107 na kumshinda, Elisha Mwandele (CHADEMA) ambaye alipata kura 1906.
Aidha katika Kata ya Nsalaga, Kasusura, alimtangaza, David Ngogo (CCM) kuwa mshindi wa kinyang’anyiro hicho kwa kupata kura 3847 na kumshinda, Reward Mshanga (CHADEMA) ambaye aliambulia kura 2506.