Ili uweze kuona televisheni au kusikiliza redio, ni lazima kuwe na maudhui ambayo yameandaliwa, kutengenezwa na kurushwa na kituo husika. Ili kufaidi televisheni na redio yako kwa kuwa na utazamaji na usikilizaji unaokidhi mahitaji yako, zingatia yafuatayo:
1. Kuwa na ratiba ya wiki ya kituo cha televisheni unachokipenda.
2. Usiwabughudhi watu wengine kutokana na matumizi yako ya televisheni na redio. Kuwa na staha kwa kutokufungulia vyombo hivyo kwa sauti kubwa na muda ambao kwa kawaida unajulikana kama sio wa kistaarabu.
3. Iwapo unatazama televisheni pamoja na jamii ya watu wengine, ndugu, familia, wafanyakazi wenzako au jamaa na washirika wako, jitahidi kuelewa mahitaji ya watazamaji wenzako.
4. Ingawaje kuna kanuni za utangazaji zinazosimamia maudhui ya redio na televisheni yanayofaa kwa vipindi na makundi fulani, kuwa makini na hakikisha kwamba watoto hawaangalii vipindi vyenye maudhui yanayofaa watu wazima tu.
5. Ukiona au kusikia maudhui yasiyofaa kwenye televisheni na redio toa taarifa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
MAMBO ANAYOJIVUNIA BABA LEVO KATIKA MIAKA YAKE MITATU