Leo December 4, 2018 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ametemlea Makao Makuu ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Jijini Dar es Salaam.
Lengo la kutembelea Kituo lilikuwa ni kukutana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIC na Menejimenti na kupokea taarifa ya mwenendo wa utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Kituo kwa sasa ili kujipanga upya katika kutekeleza majukumu hayo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Hatua hiyo ni kufuatia maelekezo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoyatoa November 12, 2018 kukihamishia Kituo cha Uwekezaji Tanzania chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Akiwa TIC, Waziri Mkuu amefanya ziara ya kutembelea Ofisi za Huduma za mahala pamoja kwa Wawekezaji ‘One Stop Facilitation Centre’ ambapo amezungumza na baadhi ya Maafisa husika kuhusu huduma wanazotoa, namna wanavyotoa na changamoto wanazokumbana nazo katika kutoa huduma hizo.
Baada ya ziara hiyo, Waziri Mkuu ameendesha kikao cha kazi na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenz wa TIC na Mejementi.
TAARIFA MPYA TOKA IKULU: RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA