Hii inatokea Bungeni Dodoma ambapo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Ashatu Kijaji aliposimama kujibu baadhi ya hoja za Wabunge waliokuwa wakichangia katika mpango wa bajeti mwaka 2019/20 na miongoni mwa mambo aliyoyaongelea ni pamoja na namna alivyokerwa kwa baadhi ya wabunge walitumia nafasi hiyo kuipotosha jamii kwa kutoa takwimu za uongo huku wakijua ni kosa kisheria.