Leo September 19, 2018 nakuletea stori kutoka nchini Uingereza ambapo imeripotiwa kuwa Prince William wa Uingereza anatarajiwa kukutana na Rais Dkt. Magufuli nchini Tanzania wiki ijayo wakati wa ziara yake ya siku saba barani Afrika.
Ziara ya Prince William ina lengo la kufuatilia juhudi zinazofanywa na taifa la Tanzania katika kukabiliana na ujangili, ulanguzi na uhifadhi wa Wanyama.
Inaelezwa kuwa Prince William atafanya ziara hiyo kama Rais wa mashirika yanayotetea uhifadhi wa Wanyama ya United for Wildlife na Tusk Trust na anatarajiwa pia kuzuru Kenya na Namibia.
Aidha Tanzania imekuwa ikifanya juhudi kukabiliana na ujangili na ulanguzi wa wanyama huku takwimu zikieleza kuwa Tanzania ilikuwa na tembo 110,000 mwaka 2009 lakini idadi hiyo imeporomoka hadi kufikia tembo 43,000 kutokana na ujangili.
Bonyeza hapa chini kusomewa Magazeti ya leo September 19 2018 na Pascal Mwakyoma.