Leo September 28, 2018 Kutoka huko Afrika ya Kusini nyuki wameingia kwenye injini ya ndege ya shirika la Mango na kusababisha kuchelewa kwa safari za ndege katika uwanja mkuu wa ndege mjini Durban.
Wataalamu wa nyuki waliitwa kuja kusaidia kuwaondoa nyuki hao zaidi 20,000 kutoka kwenye injini ya ndege hiyo.
Mmoja wa wataalamu hao amesema tukio hilo si la kawaida na kwamba huenda nyuki hao walikua wakipumzika kabla ya kuelekea mahali pengine.
Ameongeza kuwa hawakua na mpango wa kuishi ndani ya injini iliyo na ”harufu ilikuwa kali”.
Msemaji wa shirika la ndege la Mango, Sergio dos Santos amesema ”Sijawahi kuona kisa kama hiki katika kipindi cha miaka minane niliyohudumu katika shirika la ndege”
Ilichukua muda kabla ya watalamu hao kuruhusiwa kuingia ndani ya uwanja wa ndege kwa sababu walihitaji idhini kutoka kwa mamlaka ya usimamizi wa viwanja vya ndege nchini.
Melvyn Dawson, mmoja wa wataalamu wa nyuki alisema ilikua ”kazi rahisi” na kwamba walichohitaji ruhusa tu ya kufikia ndege hiyo”.
Akizungumza Dawson, alisema, “Tumekumbana na visa kadhaa vya kuondoa nyuki waliyovamia mahali fulani lakini sijawahi kuona kisa kama hiki”.
RC Mbeya achafukwa na mradi uliotengenezwa kihuni “DC, Mkurugenzi nanyi mpo mmeupokea”