Leo September 8, 2018 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) amewatembelea majeruhi wa ajali ya barabarani iliyosababisha vifo vya watu 15 na wengine kujeruhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya.
Sugu akizungumza mara baada ya kuwatembelea majeruhi amesema watu 15 kupoteza maisha ni tukio kubwa sana tena kwa ajali ya aina ile ile licha ya serikali kuendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo.
“Wakati wa watendaji na wanasiasa kukaa pamoja umefika wa kujadili na kutatua changamoto hii ya ajali na kuachana na mihemuko ya kisiasa tukae kitalaamu tujui tatizo nini’ amesema Sugu
Sugu amesema kuwa bila kuchukua hatua za kitaalumu ikiwemo kupanua barabara na si kubadilissha ma-RC, Mawaziri Mambo ya Ndani.
“Tutabadilisha ma-RC, ma-RPC na Mawaziri wa Mambo ya Ndani lakini pia ni vema kutumia watalaamu ni jinsi gani tatizo la ajali linaweza kutaliwa.” amesema Sugu