Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini, Malusi Gigaba amejiuzulu nafasi yake hiyo kufuatia kuandamwa na tuhuma za kudanganya serikali na Wananchi wa Afrika Kusini.
Rais Ramaphosa amethibitisha kujiuzulu kwa Gigaba, ikiwa ni siku moja kabla ya Rais kukutana na washauri wake, mkutano ambao unatajwa ulipanga kumchukulia hatua kiongozi huyo.
Gigaba amekuwa kwenye wakati mgumu baada ya mwezi uliopita kulazimika kuomba msamaha kutokanana na video yake binafsi ya ngono kuvuja mitandaoni.