Baada ya hivi karibuni Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kutembelea na kukagua ujenzi wa barabara za juu (flyover), eneo la TAZARA Dar es salam na kusema umekamilika kwa asilimia 98, hatimaye leo barabara hizo zimeanza kutumika.
Msemaji mkuu wa serikali Dkt. Abbas Hassan, amethibitisha kuwa kuanzia leo serikali imeruhusu rasmi matumizi ya barabara hizo hadi pale uzinduzi utakapofanyika mwezi ujao.
“Naweza kuwathibitishia kuwa leo Serikali imeamua rasmi kuruhusu magari kutumia daraja la juu la Tazara kuelekea uzinduzi rasmi utakaofanyika mwezi ujao.” Msemaji wa Serikali
Nae Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa amethibitisha hilo kupitia page yake ya Twitter. “HATIMAYE barabara ya juu inayokatiza katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela Jijini Dar es Salaam (Mfugale Flyover) yaanza kutumika. Hongera wana Dar es Salaam. Asante Mhe. Rais Magufuli.“
Mkiwaona JWTZ, FFU msishtuke | Mikono inawasha sana na tuna hamu