Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kilimanjaro imewafikisha mahakamani madiwani wawili wa CCM katika wilaya ya Same kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa wananchi.
Madiwani hao ambao ni Michael Chikira Mauya wa kata ya Myamba na Aston Elinaz Diwani wa kata ya Mpinji wamefikishwa katika mahakama hiyo na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU Suzan Kimaro, mbele ya hakimu wa mahakami hiyo Judith Kamala.
Michael Chikira anashtakiwa kwa kufanya udanganyifu wa kukusanya shilingi Milioni 7 na laki nane kutoka kwa wananchi 53 kutoka kwenye vijiji mbalimbali vya kata hiyo.
Elinaz Mgonja anashtakiwa kwa kujipatia zaidi ya Milioni tatu na laki sita katika kata ya Mpinji na Myamba kwa njia ya udanganyifu.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na taasisi hiyo zinadaiwa madiwani hao wanatuhumiwa kuwachangisha wananchi fedha shilingi laki moja na nusu kila mmoja kwa madai ya kuwafungia umeme wa REA huku madiwani hao wakiwa wanafahamu kufanya hivyo sio kweli.
Watuhumiwa hao wamekana mashtaka hayo nakuachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni mbili kila mmoja, upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na kesi hiyo itakuja kutajwa tena September 27.
“Tulimpinga Rais Magufuli kununua Dreamliner, ila ni idea nzuri nampongeza” Matiko