Old Boma ni jengo lililo karibu na Bandari ya DSM, wakati huo likiitwa Bandari Salaam chini ya utawala wa Sultan Sayed Siad wa Oman. Idadi kubwa ya wakazi wa Mji wa DSM na wasio wa Mji huo wanalipita Jengo la Old Boma kila siku huku wengi wao wakishindwa kujua kama ndio ghorofa la kwanza kujengwa.
Ghorofa hilo lilijengwa mnamo mwaka 1860 na kukamilika mwaka 1866 ambapo lilijengwa na Sultan Sayyed ama Sultan Majjid kwa ajili ya wageni wake kwa maana nyingine ilikuwa nyumba ya wageni “Guest House” lakini kwa karne ya sasa kutokana na jengo hilo kuzungukwa na majengo marefu ya thamani linaonekana si chochote mithili ya takataka.
ALIEJENGA NYUMBA MPAKANI MWA KENYA NA TANZANIA “SIJUI MIMI RAI WA WAPI”