Usiku wa September 16, 2018 Julius Kalanga ametangazwa mshindi wa kiti cha Ubunge katika Jimbo la Monduli mkoani Arusha, baada ya kupata kura 65,714 dhidi ya kura 3,187 alizopata mshindani wake Yonas Leiser wa CHADEMA.
Mwita Waitara (CCM) ametangazwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga jijini DSM kwa kura 76,292 dhidi ya Asia Msangi(CHADEMA) aliyepata kura 8,072.
Ikumbukwe kuwa Mwita Waitara na Julius Kalanga walikuwa Wabunge wa Majimbo hayo awali kupitia CHADEMA kabla ya kuhamia CCM na kugombea tena.
Bonyeza PLAY hapa chini kutazama alichoongea Mbunge Mteule wa Monduli Kalanga.
LIVE MAGAZETI: Mapambano, Bastola, panga vyanaswa kituoni, Nini kinafuata kwa Lowassa