Katika kuendelea kupambana na changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa Wilayani Korogwe Mkuu wa Wilaya hiyo Kissa Kasongwa amezindua rasmi kampeni yake ijulikanayo kwa jina la ‘NIVUSHE’ “nitimize ndoto zangu ” kampeni inayolenga kumsaidia mtoto apate elimu bora sambamba na uchangiaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe DC Kissa amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa Rais John Pombe Magufuli imeleta Sera ya elimu bure ambapo Sera hiyo imesaidia kukuza muitikio wa wazazi kuwapekeka watoto wao shule.
Aidha DC Kissa amesema kuwa kiwango cha ufaulu wa darasa la saba kimeongezeka kwa kiasi kikubwa wilayani Korogwe ambapo uwepo wa kampeni hiyo utasaidia kupunguza changamoto za uhaba wa vyumba vya madarasa ambapo kampeni hiyo itajumuisha wananchi kwa kuchangia kila mmoja shilingi mia tano.
Hata hivyo DC Kissa ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kuchangia katika kampeni hiyo ili kufakisha ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyohitajika Wilayani Korogwe.
MTOTO WA MAMA LISHE ALIEAMUA KUSOMESHA WENGINE, KUWAJENGEA NYUMBA