Leo September 28, 2018 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geophrey Mwambe amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Einar Jensen.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Mwambe amesema Balozi Jensen amekuwa mdau mkubwa katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji na kufanyabiashara.
“Balozi Jensen ni rafiki mkubwa wa biashara na amekuwa akishiriki kikamilifu katika kuandaa mazingira mazuri ya kiabiashara.Tumekuwa tukishirikiana na Balozi Jensen kuratibu za kuwezesha wafanyabiashara,” -Mwambe.
Pia amesema Balozi Jensen katika kutafuta masoko ya bidhaa za kilimo kwa kuhakikisha wakulima wanakuwa na soko la uhakika huku akieleza kwamba balozi amekuwa akihamasisha wawekezaji wa Denmark kuwekeza nchini Tanzania.
“Balozi amekubali kuisaidia TIC katika mabadiliko ya kimfumo koutendaji.Kama nchi tumedhamiria kushindana kidunia.Tunakuza uwezo wa kuongeza ajira kwa Watanzania,” amesema Mwambe
Pia wamekubaliana na Balozi Jensen katika kuandaa maeneo ya yaliyopimwa kwa ajili ya uwekezaji.“Nchini kwetu hatuna tatizo la ardhi kwani ipo ya kutosha ila changamoto ipo kupata eneo ambalo limepimwa”.
“Hivyo moja ya mipango yetu ni kuhakikisha maeneo ya uwekezaji yanapimwa na mwekezaji anapohitaji eneo inakuwa rahisi kupata.Bolozi amekubali kisaidia katika upimaji wa maeneo,” Mwambe
Mwambe amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Denmark kuna kampuni kubwa za nchi hiyo ambazo zimejenga viwanda.
Pia amesema kupitia Balozi huyo Denmark kwa sasa kuna mchakato wa mradi wa umeme wa upepo unaoendelea mkoani Dodoma.
Kwa upande wake Balozi Jensen amesema nchi hizo mbili zimekuwa kwenye ushirikiano mkubwa kwa miaka 50 na kwamba nchi ya Denmark imekuwa ikisaidia katika mambo mbalimbali yanayohusu uwekezaji.