Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola alilazimika kusimama bungeni Dodoma kutolea ufafanuzi wa Serikali kuhusu madai aliyoyatoa Mbunge wa Konde Khatib Haji kwamba Serikali inaingia kwenye mtego wa kujihusisha na matukio ya ushoga ikiwemo ndoa za aina moja.
“Viungo ambavyo mashoga wanavitumia vina kazi maalum kwa mujibu wa uumbaji wa Mungu, Serikali yetu kamwe haitaruhusu mwanadamu yeyote kubadili matumizi ya kiungo ambacho kimekusudiwa kwa ajili ya kutolea haja kitumike katika matumizi mengine ambayo Mungu hakukusudia” -Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola