Leo November 21, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi wa kesi ya kuchapisha picha za ngono na kuzisambaza kwenye mtindao ya kijamii inayomkabili msanii Wema Sepetu bado haujajamilika.
Kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na Upande wa Mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Jenipher Masue ambapo amedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika ambapo baada ya Wakili Masue kueleza hayo, Hakimu Mkazi Maira Kasonde ameahirisha kesi hiyo hadi December 12, mwaka huu kwa ajili ya kuitaja ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.
Wema anakabiliwa na kosa moja la kuchapisha picha za ngono na kuzisambaza katika akaunti yake ya Instagram ambapo miongoni mwa masharti ya dhamana, ni kutakiwa kutoweka video zinazohusiana na ngono wala maneno yoyote yenye viashiria vya kingono katika Instagram yake.
Mwigizaji Wema Sepetu anadaiwa October 15, 2018 katika sehemu tofautitofauti za Dar es Salaam alichapisha video ya ngono na kuisambaza katika akaunti yake Instagram.