Wananchi wa Kata ya Matwiga iliyopo Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya wamembana Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa atoe majibu ni lini maji yatatoka katika Kata hiyo tangu wamehaidiwa miaka zaidi ya kumi iliyopita.
Prof. Mbarawa alitembelea mradi mkubwa wa Bwawa la maji ambalo litasaidia kusambaa maji katika Kata hiyo ambapo mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 93 kukamilika ambapo ilimbidi amipigie Mtendaji wa wakala wa visima na mababwa na kumtaka ikifika April 15 wawe wamefika ili kumalizia ujenzi ambao umechukua mpaka sasa zaidi ya miaka kumi bila kuisha.