Leo March 20, 2018 stori kutoka katika Mahakama ya Kisutu ambapo Mfanyabiashara, Hariri Mohammed Hariri (45), mkazi wa Kinondoni, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin gramu 214.11
Akimsomewa mashtaka yake na Wakili wa serikali, Clara Chalwe mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja.
Inadaiwa March 2, 2018 maeneo ya Kinondoni Matitu Dar es Salaam, ambapo mshtakiwa alisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride zenye uzito wa gramu 214.11.
Baada ya kusomea shtaka hiko, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chohote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya isipokuwa kwa kibali kutoka kwa DPP.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.
Hakimu Shaidi ameahairisha kesi hiyo hadi April 4,2018.