Leo February 25, 2018 hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia Wataalam wake wa Magonjwa ya Pua, Masikio na Koo wakishirikiana na Wataalam kutoka Medel, Austria wamewawashia vifaa vya usikivu Watoto sita waliofanyiwa upasuaji na kupandikizwa vifaa maalum vya usikivu.
Watoto hao wamepandikizwa vifaa hivyo January 2018 Muhimbili. Kuwashwa kwa vifaa hivyo kutawawezesha kwa mara ya kwanza watoto hao kusikia na wataanza maisha mapya ya kusikia sauti mbalimbali katika mazingira yanayowazunguka.
Kwa mujibu wa wataalam wa Muhimbili kumpeleka mtoto mmoja nje ya nchi kupandikizwa kifaa hicho gharama uwa kati ya Shilingi Milioni 85 hadi Milioni 100 wakati gharama kwa mtoto mmoja Muhimbili ni Milioni 33.
RPC Kinondoni amezungumza kuhusu Majeruhi wa Risasi waliopo OYSTERBAY Polisi