Mamlaka nchini Ukraine zilidanganya kuwa mwanahabari Arkady Babchenko ameuawa ili kuzuia jaribio la kweli la kutaka kumuua, mkuu wa shirika ya usalama Ukraine, Vasyl Hrytsak, amesema.
kifo chake kiligonga vichwa vya habari vya kimataifa Jumanne usiku, amejitokeza katika kikao cha waandishi wa habari jana akiwa mzima wa afya, mwanahabari huyo alivishukuru vyombo vya usalama vya Ukraine kwa kuyaokoa maisha yake.
Mkuu wa idara ya usalama ya Ukraine Vasily Gritsak alidai kuwa maafisa wa ujasusi wa Urusi walimpa mwanaume mmoja wa Ukraine dola 40,000 kufanya mauaji ya mwanahabari huyo wa Urusi anayeishi uhamishoni.
Kifo hicho kilipangwa na mwanahabari huyo na polisi ya Ukraine baada ya kupokea vitisho vya kuuawa. Polisi wamesema mshukiwa mmoja amekamatwa.