Leo June 1, 2018 Kuna hii stori ya kuifahamu Wakazi 80 wamekamatwa na jeshi la polisi baada ya kukosa vyoo kwenye makazi yao katika wilaya ya Budaka nchini Uganda .
Kwa mujibu wa Inspekta wa afya wa wilaya hiyo Max Oswamu amedai kuwa wakazi hao wanatumia vichaka kujisaidia kitu ambacho ni hatari kwa afya zao.
Wilaya hiyo ndio inakadiriwa kuwa na vyoo vichache nchini humo na hao watuhumiwa 80 walikamatwa alhamisi hii katika operesheni iliyoendeshwa na idara ya afya wilayani humo kwa kushirikiana na jeshi la polisi.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Sam Mulomi amesema kuwa “wamegundua kuwa watu wengi ikiwemo viongozi waliosoma hawana vyoo kwenye makazi yao.Na hawawezi kuwa viongozi halafu wakose na choo”.
Aidha watuhumiwa hao kwa sasa bado wanashikiliwa na jeshi la polisi katika kituo cha polisi Mugiti na kwa mujibu wa Inspekta Oswamu watuhumiwa hao watakuwa fundisho kwa watu wengine wasiokuwa na vyoo katika makazi yao.