Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata Diwani wa CHADEMA kata ya Endamaratiek, John Lucian, kwa tuhuma za kula Milioni 54 za halmashauri ambazo anadaiwa alizichukua mwaka 2013 ikiwa ni miongoni mwa fedha za mkopo wa Halmashauri toka Bank ya TIB kwaajili ya ujenzi wa kiwanda cha maziwa.
Gambo ametoa agizo hilo kufuatia Diwani Huyo kudaiwa kutolipa fedha hizo na jambo hilo limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu na Halmashauri ya Karatu.
Gambo pia ameagiza kuhamishwa kwa Mhasibu Colex Andongalile na Afisa mipango Fidelis Neneywa wa Halmashauri ya Karatu kwa kudaiwa kukwamisha baadhi ya shughuli za kimaendeleo.