Leo June 5, 2018 Serikali ya Burundi imethibitisha kuwa sherehe za utiaji sahihi kwenye katiba mpya na kuitambulisha kwa raia zitafanyika alhamisi katika mkoa wa kati wa Gitega eneo la Bugendana.
Eneo la Bugendana ndiko kulizinduliwa rasmi mchakato wa katiba na pia kampeni ya chama madarakani CNDD/FDD ya kuipiga debe katiba hiyo.
Itakuwa mara ya kwanza katika historia ya Burundi kuwa na sherehe za kuipokea katiba mpya
Hata hivyo wapinzani na baadhi ya nchi za kigeni wamekosoa mchakato huo mzima kwamba haukuzingatia sheria na katiba mpya inanuwia kumbakiza madarakani Rais Pierre Nkurunziza hadi mwaka 2034.