Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema itaifuta kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais wa Tanzania, John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee kwa sababu ya shahidi kushindwa kutoa ushahidi kwa zaidi ya mara tatu.
Hayo yameelezwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa Serikali, Silivia Mitato kudai kuwa Wakili anayeendesha shauri hilo amepangiwa kazi nyingine hivyo anaiomba mahakama impe muda ili apitie jalada hilo.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba amesema kumbukumbu zake zinaonyesha shahidi Abdull Chembea amefika mahakamani hapo zaidi ya mara tatu na hajawahi kutoa ushahidi, hivyo tarehe ijayo kama haijaanza kusikilizwa anaweza kuifuta.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi August 28 na Septemba 4, 2019 kwa ajili ya kusikilizwa.
MAGUFULI ATINGA NYUMBANI KWA MBOWE, WAMEKAA KITI KIMOJA