Leo June 4, 2018 Jamaa mmoja ambaye hakutambulika jina, katika hali ya kushangaza alimvamia mwanamke mmoja aliyekuwa katika kituo cha bus jijini Goiania nchini Brazil na kumkata nywele zake kisha akakimbia nazo kusikojulikana.
Inspekta Jose Carlos Bezerra da Silva amesema kuwa, mwanamke huyo alikuwa akisubiria gari na ndipo alipotokea jamaa huyo akiwa na kisu kisha akazikata nywele za mwanamke huyo ambazo zilikuwa zinakaribia kufika kiunoni na kutokomea sehemu isiyojulikana.
Aidha mwanamke huyo alidhani kuwa jamaa alitaka kumpora pochi yake yenye fedha kumbe lengo la mwizi huyo lilikuwa tofauti..
Polisi walisema kuwa nywele hizo za mwanamke huyo zilikua ni nywele asilia hivyo inawezekana jamaa huyo ameziiba ili aende akawauzie wanaotengeneza ‘Wigs’.