Uganda wanafikiria kuvutia Watalii wengi duniani kwenda nchini humo kwa kujenga Makumbusho ya Vita ya Uganda itakayokuwa na historia na taarifa zote za nchi hiyo katika kipindi kibaya cha historia ya Uganda.
Katika Makumbusho hayo Mauaji na maovu yote yaliyotendeka wakati wa miaka 8 ya utawala wa Rais wa zamani wa nchi hio Nguli Idi Amin pamoja na jeshi la waasi Lord’s Resisitance Army (LRA) yataoneshwa.
“Tunataka kuweka kumbukumbu na historia ya taifa hili wazi” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa wa Bodi ya Utalii ya Uganda Stephen Asiimwe.
Katika Makumbusho hayo ya Vita ya Uganda kutakuwa pia na historia ya taifa hilo kabla ya ukoloni na wakati wa ya ukoloni.
“Historia inakuwa utajiri kadri siku zinavyokwenda na kuwa ya kuvutia kama mvinyo” aliongeza Asiimwe huku akiweka sawa kuwa Makumbusho hayo hayana nia ya kuamsha hisia mbaya na kupotosha watu juu ya historia ya nchi hio.
Hata hivyo baadhi ya taarifa zinazomuhusu Idi Amin ambazo zitakuwepo kwenye makumbusho hayo ni pamoa;
- Alijiunga na jeshi la King’s African Rifles akiwa kwenye miaka ya 20
- Alichukua madaraka mwaka 1971
- Watu takribani 400,000 wanadaiwa kuuawa katika utawala wake
- Mwaka 1972 aliwafukuza watu wote wa jamii kutoka bara la Asia akiwatuhumu kwa kushusha uchumi wa nchi hiyo
- Alibadili dini na kuwa Muislamu na kuoa wake watano na kufanikiwa kupata watoto wengi huku akisisitiza kuitwa ‘Bigg Daddy’
- Alijitangaza kama Mfalme wa Uskochi na kuzuia uvaaji wa nguo fupi
- Mwaka 1979 aliondoshwa na majeshi ya Tanzania na kukimbia nchi
- Na mwaka 2003 alifariki nchini Saud Arabia
Aidha John Sempebwa ambaye ni makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Muongozaji wa Bodi ya Utalii ya nchi hiyo amesema kuwa anawakatalia wale wote wanaosema kuwa nchi hio inataka kuwarejeshea maumivu wananchi wake yanayotokana na matukio ya huko nyuma kwa kujenga kwa Makumbusho hayo.
Matokeo ya Mtoto aliyemshtaki Baba yake yametoka, anazungumza Kiingereza