Leo May 28, 2018 Nakusogezea stori kutoka katikaambapo Mahakama ya juu nchini Misri imeamuru mtandao wa YouTube ufungwe kwa mwezi moja nchini humo kwa kuonyesha video inayomkufuru mtume Muhammad.
“Uamuzi huo ni wa mwisho na hakuna anayeweza kukata rufaa,” wakili Mohamed Hamed Salem aliyewakilisha kesi hiyo mahakamani aliambia shirika la habari la Xinhua.
Hapo awali mahakama ya nchini humo iliagiza halmashauri ya mawasiliano nchini Misri (NTRA) kufunga YouTube lakini NTRA ikakata rufaa ikisema kwamba haina uwezo wa kisheria.
Wakili Hamed Salem aliyewakilisha kesi hiyo mahakamani mwaka wa 2013 alipendekeza mahakamani kwamba mtandao huo wa YouTube ufungwe na kupigwa marufuku nchini Misri hadi utakapoondoa video hiyo inayomkufuru mtume Muhammad na video zingine zinazoenda kinyume na imani ya dini ya Kiislamu.