Nchini Hispania kuna tamasha linaitwa ‘Near Death Festival’ ambalo hufanyika kila mwaka katika mji wa Las Nieve nchini humo ambapo baadhi ya watu waliokuwa karibu kufa kutokana na sababu mbalimbali hubebwa kwenye majeneza na kutembezwa kwenye mitaa ya mji huo.
Siku ya adhimisho la tukio hilo mamia ya watu huenda kusali katika kanisa la Mtakatifu Marta wa Ribarteme kisha baada ya kusali, watu ambao kifo kiliwanyemelea katika kipindi cha miezi 12 iliyopita hubebwa kwenye majeneza na kutembezwa katika baadhi ya mitaa ya mji huo kama ishara ya kuonesha shukrani kwa kunusurika na kifo.