Leo June 7, 2018 nakusogezea stori kutoka kwa amabapo Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage ameipongeza kampuni ya mafuta ya Total kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kuhakikisha kuwa watanzania wanapata mafuta bora ya vyombo vya moto.
Mwijage amezungumza jijini DSM kwenye uzinduzi wa mafuta ya vyombo vya moto aina ya Total Excellium kutoka kampuni hiyo. Mafuta hayo yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya ubora wa juu ya kimataifa kwa bidhaa zinazotumia mafuta ya Petroli na Diesel katika soko la Tanzania.
“Uzinduzi wa mafuta haya umekuja wakati muafaka kwani sasa tuko kwenye wiki ya mazingira na mafuta haya yanapunguza uchafuzi wa hali ya hewa utokanao na vyombo vya moto, nawapongeza kwa kuwaletea watanzania bidhaa bora na mimi na utaalamu wangu wa mafuta nafahamu hii ni hatua kubwa sana kwenye teknolojia ya kuboresha mafuta,” alisema Mwijage.
Mafuta haya mapya yana uwezo wa kusafisha injini na kuwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu, kuwezesha matumizi kidogo ya mafuta na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa utokanao na moshi wa vyombo vya moto.
Tarik Moufaddal, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Total nchini amesisitiza, “Kuzinduliwa kwa Tola excellium, katika soko la Tanzania ni hatua mpya na muhimu kwetu nchini hususani katika kufanikisha dhamira yetu ya kuingiza bidhaa bora za nishati.”
“Total excellium imetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ambayo inawezesha kusafisha injini, kuwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu bila kuchoka, kupunguza uchafuzi wa mazingira utokanao na moshi na ni mazuri kwa matumzi ya aina zote za magari kuanzia madogo mpaka makubwa,” aliongeza Tarik.
FULL STORY: Producer aeleza dakika za mwisho za maisha ya ‘SAM WA UKWELI’