Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Kilimanjaro imewafikisha mahakamani watumishi watatu wa Halmashauri ya Mwanga kwa tuhuma za kutenda makosa manne.
Akiwasomea mashtaka hayo mwanasheria wa TAKUKURU, Suzan Kimaro amesema watuhumiwa hao wanadaiwa kughushi, kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri, ubadhirifu na kutenda kosa chini ya sheria ya kupambana na rushwa.
Watuhumiwa hao ambao ni Hassan Mkwizu, Mustafa Haji pamoja Monika Mkasi wanadaiwa kufanya ubadhirifu wa Milion 11 nakusema waliwalipa walinzi kwenye uchaguzi mkuu wa Urais madiwani na wabunge wa mwaka 2015.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Mariam Kito amewaachia watuhumiwa hao kwa dhamana ya Milion 6 ambapo kesi itatajwa tena July 7.