Leo June 5, 2018 Stori ya kuifahamu ni kutoa nchini ya Saudi Arabia ambapo June 4, siku iliwapa wanawake leseni ya kuendesha gari baada ya miongo kadhaa ya kupiga marufuku.
Nchi hiyo ilitangaza wiki iliyopita kuwa iko tayari kuwaruhusu wanawake kuendesha magari, kuanzia June 24, baada ya Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud kutoa amri mwezi wa September mwaka jana ya kuwaruhusu wanawake kuendesha magari.
Waziri wa Mambo ya Ndani Msaidizi, Jenerali Saeed Al-Qahtani alithibitisha kwamba wanawake wote walio na uwezo wa kuendesha gari wako huru kuendesha gari.