Leo May 22, 2018 ninakusogezea stori kuhusu Makampuni ya teknolojia ambapo mwaka huu yametajwa kuongoza kwenye orodha ya makampuni yenye mapato makubwa zaidi nchini Marekani huku Apple, Amazon, Alphabet, Microsoft na IBM yakiwemo katika makampuni 50 bora.
Katika orodha hiyo ya “Fortune 500” ambayo huchapishwa kila mwaka na jarida la “Fortune”, kampuni ya Apple iliibuka katika nafasi ya 4 ikiongoza makampuni ya teknolojia na mapato ya dola Bilioni 48 licha ya kupungua kwa mapato yake kwa 6%.
Kampuni ya Amazon kwa mara ya kwanza ilitokea miongoni mwa makapuni 10 bora kwenye nafasi ya 8.
Makampuni ya Apple, Alphabet na Amazon yanaongoza miongoni mwa makapuni bora ya teknolojia yakifuatwa na Berkshire Hathaway, Facebook,na JPMorgan Chase kulingana na orodha hiyo. Makapuni tano bora kwenye orodha ya “Fortune 500” mwaka huu ni Walmart, Exxon Mobil, Berkshire Hathaway, Apple na UnitedHealth Group.