Usiku wa kuamkia January 21, 2018 Watu wenye silaha za kivita wamevamia hoteli ya Intercontinental katika Mji mkuu wa Afghanistan Kabul na kuwafyatulia risasi wageni na wahudumu wa hoteli hiyo pamoja na kuichoma moto.
Vikosi vya usalama vimepambana nao kwa zaidi ya saa nane. Naibu wazizi wa mambo ya ndani Nasrat Rahimi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba washambuliaji wawili kati yao wameuawa.
Hakuna aliyejitokeza kudai kuhusika na shambulio hilo, katika mji mkuu wa Afghanistan ulioharibiwa kwa vita na ambako kumekuwa kukitolewa maonyo ya mfululizo siku za karibuni ya kuwataka watu kuepuka hoteli na maeneo mengine yanayotembelewa na wageni.
Haijulikani watu wangapi bado wamekwama ndani ya hoteli hiyo, ambayo iliwahi kuvamiwa na kundi la Taliban mnamo mwaka 2011, au kama kuna raia wowote wa kigeni miongoni mwao.
KIJANA WAKITANZANIA ALIYEJENGA SHULE YA BILIONI 1.4, JINSI ALIVYOKUSANYA FEDHA ZA UJENZI