Wakati akijibu tuhuma dhidi yake kuhusu kuomba rushwa, Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya alidai kuwa tuhuma hizo zilizotolewa na Mfanyabiashara mmoja zilitokana na Mfanyabiashara huyo kuzuiwa kupora ardhi ya Bi. Maria Kiriwa mkazi wa Hai.
Baada ya Bi. Kiriwa kuonekana akithibitisha kutaka kuporwa ardhi na Mfanyabiashara huyo, Watu mbalimbali walidai kuwa Bibi huyo ametengenezwa ili kumchafua Mfanyabiashara huyo, huku wakidai kuwa ni mkazi wa Jijini Arusha maarufu kama ‘Chalii wa R Chugga’.
Hatimaye leo ‘Chalii wa R Chugga’ ameonekana akizungumzia madai hayo.