Rais John Pombe Magufuli amemwagiza Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Isaack Kamwelwe kuitisha mapema iwezekanavyo zabuni ya ujenzi wa kivuko kipya ili wananchi wa Bugolora na Ukara wapate huduma nzuri baada ya kile cha MV Nyerere kuzama.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiongea kwenye eneo la tukio huko Ukara, Ukerewe, ambapo amesema pamoja na maamuzi ya kuvunja bodi ya TEMESA na kutengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya SUMATRA, lakini pia Rais Magufuli ameagiza ujenzi wa kivuko kipya, kitakachohudumia wakazi wa eneo la Ukara na Bugolora.
”Rais ameagiza leo Waziri aitishe zabuni ya ujenzi wa kivuko kipya chenye uwezo wa kubeba tani 50, na abiria zaidi ya 200 na itakuwa na uwezo mara mbili ya Mv Nyerere pia kiwe na uwezo wa kufanya safari nyingi ili kuepusha kuzidisha watu”.
Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi SUMATRA