Rais John Magufuli amesema amewasamehe wabunge January Makamba na William Ngeleja waliomuomba msamaha baada ya sauti zao wakiwa wanazungumzia masuala mbalimbali kusambaa katika mitandao ya kijamii.
“Hivi karibuni kuna watu walinisema sema kwenye mitandao nikajiuliza hawa watu wakipelekwa central watapinga kweli, lakini wakaja wawili kuniomba msamaha akiwemo January Makamba na Ngeleja nikawasamehe nikaona ni vijana, nimewasamehe na nimesahau tujifunze kusamehe” Rais Magufuli