Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Jonathan Shana ameelezea chanzo cha awali walichobaini kufuatia Mkurugenzi wa fedha na Mipango katika hospitali ya Rufaa Bugando Suzan Bathlomeo kufariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofani.
Kamanda Shana amesema katika ofisi ambayo alikuwa anaiongoza Marehemu Suzan kulikuwa na upotevu wa fedha zaidi Milioni 300 na tayari baadhi ya wenzake wameshafukuzwa kazi.
Mkurugenzi wa Fedha Bugando ajirusha toka ghorofani afariki dunia