Leo June 29, 2018 Mahakama ya Mombasa imewatia hatia polisi wa Kenya kuhusika katika kifo cha Alexander Monson, raia wa Uingereza aliyeshutumiwa kutumia madawa ya kulevya na ambaye alikutwa amekufa gerezani mwezi May 2012 katika mji wa Diani kusini mwa Kenya.
Kwa upande wa familia yake, wamesema kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 alipigwa hadi kufa, wakati ambapo polisi imedai kuwa alikufa kwa kwa kutumia kiwango kikubwa cha dawa ya kulevya aina ya Cannabis, hoja ambayo imefutiliwa mbali na mahakama.
“Kifo chake hakikuwa cha kawaida na hakikusababishwa na madawa ya kulevya, maisha yake yalifupishwa na polisi,” amesema Jaji Richard Odenyo, ambaye amebaini kwamba maafisa wanne wa polisi wanapaswa kushtakiwa kwa mauaji. ya Monson.
Mwendesha Mashtaka Mkuu Noordin Haji ameamuru kukamatwa kwa afisaa wanne wa polisi.
MAGAZETI LIVE: Biashara ya kushikwa nyeti, matiti yaibuka, Mateso ya korosho