Mhudumu mmoja amefukuzwa kazi kwenye mgahawa mmoja nchini Japani baada ya kudaiwa kutengeneza cocktail na Kisha kuichanganya damu yake mwenyewe kwa ombi la mteja anayelipia kinywaji hicho.
Mfanyakazi huyo ambaye jina lake halikujulikana alidaiwa kuingiza damu yake kwenye menyu kuu, inayoitwa orikaku, ambayo kwa kawaida hutengenezwa kwa matunda au sharubati.
Kulingana na tafsiri iliyoripotiwa hapo awali, wasimamizi wa mgahawa, ambao walilinganisha vitendo hivyo sawa na “ugaidi wa kazini,” walifunga biashara hiyo kwa siku moja ili kuchukua nafasi ya glasi zote zilizochafuliwa na kutupa chupa zozote za pombe zilizokuwa na damu na baadae Wasimamizi waliomba msamaha hadharani, wakitaja vitendo vya kuchanganya damu na kinywaji havikubaliki kabisa.
Mmiliki wa mgahawa huo uliofunguliwa mwezi uliopita, uko katika mji wa Sapporo, huko Hokkaido, gazeti la Straits Times liliripoti Kuwa alituma msamaha wake mwenyewe kwa mwathiriwa wa tukio hilo mnamo Aprili 2, akiandika “Kwa mara nyingine tena, samahani sana kukuletea shida.”
Dk. Zento Kitao aliambia tovuti ya habari ya Japan Flash, kulingana na jardin la Straits Times kuhusu tulip hilo;
“Kunywa damu ya watu wengine ni kitendo hatari sana,”
“Kesi za watu kuambukizwa kutokana na kunywa damu ya mtu mwingine ni nadra, lakini magonjwa makubwa yanaweza kuambukizwa kupitia damu, ikiwa ni pamoja na VVU, hepatitis C, hepatitis B na kaswende,Ikiwa kuna majeraha mdomoni, ni rahisi kuambukizwa na uhamishaji wa damu.”aliongeza.
Katika mazingira ya kimatibabu, alibaini, wataalam wa matibabu huchukua tahadhari zaidi na aliwataka hadharani mhudumu na wateja waliotumia kinywaji hicho chenye damu yake kupimwa kila aina ya magonjwa yanayoenezwa na damu.