Leo September 4, 2019 Mahakama Kuu ya jimbo la Gauteng imeamuru ndege ya Air Tanzania iliyokuwa ikishikiliwa nchini Afrika Kusini kuachiwa mara moja.
Na kwa taarifa za awali zinasema ndege hiyo ipo njiani kurejea Dar es Salaam ikitokea katika uwanja wa ndege wa OR Tambo jijini Johannesburg.
“Mahakama Kuu ya Gauteng, Afrika Kusini, leo imetoa hukumu na kuamuru kuwa ndege ya iliyokuwa ikishikiliwa nchini humo iachiwe na mlalamikaji alipe gharama za kesi. Tunawashukuru wote kwa uvumilivu wenu” Msemaji Mkuu wa Serikali