Rais John Magufuli amefunga mnada wa korosho kwa kuzitaka kampuni 13 zilizotaka kuzinunua kusitisha uamuzi huo kwani serikali itazinunua zote kwa bei ya Shilingi 3,300 kwa kilo moja.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo, Ikulu jijini DSM wakati akiwaapisha mawaziri na naibu waziri aliowateua Jumamosi wiki iliyopita.
“Waambie waache, watakuja kutuchezea watakwambia wanataka tani 200,000 lakini baadaye wataanza kutuleteza masharti, wamesema watanunua kwa bei elekezi Sh 3,000 je, ikipanda Desemba?” Rais Magufuli
“Kwa hiyo wanaokuja waambie waache sasa ni saa 5:12, nimeshafunga wala wasije korosho tutanunua wenyewe” Rais Magufuli
“Nimepiga hesabu mimi si mchumi korosho iliyobanguliwa ni kati ya Sh 3,000 na korosho ambazo zinategemewa kupatikana mwaka huu ni tani zaidi ya laki mbili,” Rais Magufuli
“Ile Korosho hatutonunua kwa Elfu tatu, tutanunua kwa Elfu tatu mia tatu’ Rais Magufuli