Tanzania imefungua Ofisi ndogo ya kibalozi Hongkong nchini China ambayo itahudunia masuala ya Kidiplomasia na kuongozwa na Balozi wa heshima wa Tanzania Dkt Annie Wu aliyeteuliwa September 2 , 2018 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharik.
Ofisi hiyo mpya katika Jiji la Hongkong nchini China itasimamia masuala ya kibalozi na kuwasogezea karibu huduma hizo tofauti na awali ambapo huduma za kibalozi zilikuwa zinapatikana Beijing.
Akizungumza Jijini Hongkong nchini China wiki iliyopita Balozi wa Tanzania nchini humo Mbelwa Kairuki amesema ni fursa kwa watanzania na wachina kutumia Ofisi ya Hongkong katika kupata mbalimbali kwa urahisi.
Kwa upande wake Balozi wa heshima wa Tanzania nchini China Dkt Annie Wu ameonesha kufurahishwa na kuaminiwa na Serikali ya Tanzania kwa majukumu hayo ya heshima aliyopewa na kuihakikishia Serikali kuwa pamoja na mambo ya kidiplomasia ataitangaza Tanzania kwa wawekezaji ili kuvutia wawekezaji zaidi.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania TIC Geoffrey Mwambe amesema kufunguliwa kwa Ubalozi huo kutasaidia kuongeza uwekezaji zaidi Kwani wafanyabiashara wa China watatumia Ubalozi huo katika kufuatilia masuala ya uwekezaji.
Balozi Dkt Annie Wu ambaye ni mtu mashuhuri nchini China na Hongkong anasifiwa kwa kuitangaza Tanzania kwenye mbalimbali ya kibiashara na uwekezaji pia aliwahi kuandaa makonganamo ya kibiashara yaliyojenga mahusiano ya uwekezaji baina ya China na Tanzania ambapo atahudumu kwenye nafasi hiyo ya heshima mjini Hongkong kwa Miaka mitano.
Kwa mujibu wa kituo cha uwekezaji Tanzania TIC China inaendelea kuongoza duniani kwa kuweka mitaji mikubwa nchini Tanzania kwa Za zaidi ya dola bilioni 5.8 kuanzia Mwaka 1990 mpaka mwaka 2017,ambapo kuna jumla ya miradi 723 huku ikitoa ajira 87,126.
Takwimu Hizo za kituo cha uwekezaji Tanzania TIC zimebainisha kuwa China inaendelea kuwa nchi yenye lengo la kuwekeza zaidi katika maeneo mbalimbali hapa nchini yakiwepo ya Kilimo, viwanda, Utalii, Ujenzi, teknolojia ya Mawasiliano na maeneo mengineyo.